
Mashapo ya Mafuta kwenye Mshipa wa Moyo
Kwa kawaida, mishipa ya moyo hubeba damu yenye oksijeni hadi kwenye moyo. Kwa ugonjwa wa mishipa inayosambaza oksijeni kwenye moyo, mafuta hujilimbikiza kwenye kuta za mishipa hiyo na kuzuia mzunguko wa damu. Upungufu huu katika usambazaji wa damu husababisha misuli ya moyo kukosa oksijeni na hudhuru tishu za moyo (zilizoonyeshwa kwa kijivu).