Baadhi ya Dawa Zinazotumika Kutibu Maambukizi ya Kuvu Ukeni

Baadhi ya Dawa Zinazotumika Kutibu Maambukizi ya Kuvu Ukeni

Dawa

Kipimo

Krimu, jeli, au vidonge vya kutiwa ukeni, zinapatikana bila agizo la daktari*

Butoconazole

Krimu inayotolewa kwa muda mrefu ambayo hupakwa mara moja

Clotrimazole

Inatumika kama krimu mara moja kwa siku kwa siku 7 hadi 14 au kwa siku 3, kulingana na nguvu (ukolevu)

Miconazole

Inatumika kama krimu mara moja kwa siku kwa siku 7 au kwa siku 3, kulingana na nguvu (ukolevu)

Pia inapatikana kama kidonge cha kutia ukeni kinachoingizwa mara moja kwa siku kwa siku 7, kwa siku 3 au mara moja tu, kulingana na nguvu (ukolevu)

Terconazole

Krimu zinazotumika kwa siku 3 au 7, kulingana na nguvu au vidonge vinavyoingizwa ukeni mara moja kwa siku kwa siku 3, vinapatikana ikiwa daktari ameagiza

Tioconazole

Inatumika kama dawa ya kupaka mara moja tu

Dawa zinazomezwa, zinapatikana baada ya agizo la daktari

Fluconazole

Tembe moja inayomezwa mara moja tu

*Inapatikana bila agizo la daktari isipokuwa kama imeainishwa vinginevyo.