Salama Kulala: Kupunguza Hatari ya Ugonjwa wa Kifo cha Ghafla cha Watoto Wachanga (SIDS)

Salama Kulala: Kupunguza Hatari ya Ugonjwa wa Kifo cha Ghafla cha Watoto Wachanga (SIDS)
  • Mkao wa kulala: Mlaze mtoto chali kila mara anapolala. Kulala kifudifudi, kulala kwa upande, na kutegemeza si salama.

  • Sehemu ya kulalia: Mweke mtoto kwenye sehemu imara na tambarare ya kulala, kama vile godoro la kitanda lililoidhinishwa kuwa salama, lililofunikwa na shuka iliyofungwa. Sehemu haipaswi kuwa na pembe au kwenye mteremko.

  • Kulisha: Mpe mtoto maziwa ya binadamu kwa miezi 6 ya kwanza ikiwezekana.

  • Matandiko: Weka vitu laini, mito, vizuizi vya kuzuia kuumia kitandani, vitu vya watoto kuchezea, wanyama wanasesere, blanketi zilizolegea, shuka zisizofungwa, vifuniko vya magodoro, vifaa vinavyofanana na manyoya, mashuka, vitambaa vya kufariji, na blanketi zenye uzito, vitambaa vya kufulia, au vitu nje ya sehemu ya kulala ya mtoto.

  • Kuvuta sigara hakuruhusiwi: Usiruhusu kuvuta sigara au kuvuta mivuke karibu na mtoto. Uvutaji sigara, nikotini, pombe, bangi, opioidi, na matumizi ya dawa haramu za kulevya yanapaswa kuepukwa wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua. Walezi hawapaswi kutumia dawa haramu za kulevya au pombe.

  • Eneo la kulala: Weka eneo la kulala la mtoto karibu lakini tofauti na eneo la kulala la wazazi/walezi na watoto wengine. Inashauriwa kwamba watoto wachanga walale katika chumba cha wazazi/walezi karibu na kitanda cha wazazi/walezi lakini kwenye sehemu tofauti iliyoundwa kwa ajili ya watoto wachanga, ikiwezekana kwa muda usiopungua miezi 6 ya kwanza.

  • Matitibandia: Unaweza kumpa mtoto titibandia safi na kavu la kutuliza unapomlaza chini kila wakati alale. Kwa watoto wachanga wanaonyonyeshwa, subiri umpe titibandia la kutuliza hadi unyonyeshaji utakapokuwa umeimarika.

  • Halijoto: Usimruhusu mtoto awe na joto jingi sana wakati wa kulala. Epuka kumfunika mtoto kupita kiasi, kumfunika kichwa au uso wakati wa kulala, au kumvalisha kofia akiwa ndani ya nyumba. Mpe mtoto joto kwa kutumia nguo badala ya blanketi na vifaa vingine vya kufunika. Unaweza kutumia blanketi linaloweza kuvaliwa. Usimuache mtoto peke yake ndani ya gari, bila kujali halijoto ya nje ikoje. 

  • Utunzaji wa kabla ya kujifungua: Pata huduma ya matibabu ya mara kwa mara katika kipindi chote cha ujauzito ili kupunguza hatari ya SIDS. 

  • Chanjo: Fuata mwongozo wa chanjo unaotolewa na madaktari na wataalamu wengine wa afya. Watoto wachanga wanaopokea chanjo wana hatari ndogo ya kupata SIDS. Chanjo pia hulinda watoto wachanga kutokana na magonjwa.

  • Vichunguzi na vifaa vingine: Usitumie vifaa vya kupima moyo, mwendo, au kupumua nyumbani kama njia ya kupunguza hatari ya SIDS. Vichunguzi vya nyumbani na bidhaa zinazodai kuzuia SIDS haziizuii.

  • Muda wa kulala kifudifudi: Ili kukuza ukuaji na kusaidia kuzuia madoa tambarare yasije yakatokea kichwani mwa mtoto, laza watoto wachanga kifudifudi wakati hawajalala na kuna mtu anawaangalia (muda wa kulala kifudifudi). Vipindi vifupi vya muda wa kulala kifudifudi vinaweza kuanza muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini. Muda wa kulala kifudifudi unapaswa kuongezeka mara kwa mara hadi angalau dakika 15 hadi 30 kwa siku mtoto anapokuwa na umri wa wiki 7.

Imechukuliwa kutoka kwenye The National Institute of Child Health and Human Development'sWays to Reduce Baby’s Risk.

Imechukuliwa kutoka kwenye The National Institute of Child Health and Human Development'sWays to Reduce Baby’s Risk.