Endometriosis: Tishu Isiyo Mahali Pake
Katika endometriosisi, vipande vidogo au vikubwa vya tishu za endometriamu, ambavyo kwa kawaida hupatikana kwenye utando wa uterasi (endometriamu), huonekana katika sehemu nyingine za mwili. Jinsi na kwa nini tishu hizi huonekana katika sehemu nyingine bado haijulikani.
Sehemu za kawaida ambapo tishu za endometriamu zinazopatikana sehemu isiyofaa huwa ni pamoja na ovari na mishipa inayoshikilia uterasi na, mara chache sana, mirija ya uzazi. Lakini tishu zinazopatikana sehemu isiyofaa zinaweza pia kuonekana katika sehemu nyingine za fupanyonga na tumbo au, mara chache sana, kwenye utando unaofunika mapafu au moyo.
Tishu za endometriamu zinazopatikana sehemu isiyofaa zinaweza kusababisha kuwashwa kwa tishu zilizo karibu na kusababisha bendi za tishu zenye kovu (viambatisho) kuundwa kati ya viungo vilivyo kwenye eneo la tumbo. Tishu zinazopatikana sehemu isiyofaa pia zinaweza kuziba mirija ya uzazi, na hivyo basi kusababisha utasa.
